MAADA: UANDISHI
INSHA
Insha ni kifungu cha maneno au maandishi yanayoelezea juu ya jambo Fulani, kuelezea uzuri wa kitu, mtu au mazingira Fulani. Insha za hoja ni insha ambazo huelezea jambo Fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake. Katika uandishi wa insha za aina hii mwandishi hutakiwa kuonyesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zinazotolewa zipate kueleweka sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ilio sahihi kiasi kwamba mtu asomapo insha hiyo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anajadili, na ana msimamo gani kuhusu hoja anayoielezea.Muundo wa Insha Insha za hoja kama ilivyo kwa insha ya wasifu, muundo wake una sehemu nne ambazo ni;
- Kichwa- Kichwa cha habari cha insha huandikwa kwa herufi kubwa juu ya insha katikati ya karatasi kwa kutumia maneno yasiyozidi matano.
- Utangulizi- Utangulizi wa insha ni maelezo mafupi yanayoelezea mada inayojadiliwa katika insha. Kwa kawaida utangulizi wa insha hautakiwi kuzidi aya moja.
- Kiini cha insha- Sehemu hii ya insha ndio mada yenyewe hujadiliwa, katika sehemu hii mwandishi huonyesha dhahiri jambo gani ambalo anapenda lieleweke kwa msomaji na hutoa hoja tofauti tofauti zinazotetea msimamo wake.
- Mwisho- Mwishoni mwa insha kunakuwa na maelezo ya msisitizo kuhusu jambo lililojadiliwa katika insha. Hapa mwandishi hurejea kwa muhtasari baadhi ya hoja zilizotolewa katika sehemu ya kiini cha insha.
Mambo mengine ya kuzingatia katika uandishi wa insha za hoja kama ilivyo kwa aina nyingine za insha na pamoja na uzingatiaji wa matumizi sahihi ya alama za vituo na lugha kwa ujumla. Alama za vituo amabazo hutumika mara nyingi katika uandishi wa insha ni kituo(.), alama ya mkato(,), Alama ya kuuliza(?) na alama ya mshangao (!). UANDISHI WA BARUA RASMI Barua ni karatasi yenye maandishi ya leo beba ujumbe fulani na ujumbe huo unaweza kuwa rasmi au sio rasmi, hii hutegemea na jambo linalohusiana na barua yenyewe. Dhamira kuu ya barua katika maisha ya kila siku ni kuwezesha watu kuwasiliana pale ambapo watakuwa mbali na hawawezi kuonana kwa muda mrefu. Vilevile hutumika kama njia ya mawasiliano yanayofanyika kwa siri kati ya mwandishi na mwandikiwa.Barua Rasmi Barua rasmi ni baru mambazo zinahusu mambo rasmi au ya kiofisi ambayo huhitaji mawasiliano kwa njia ya maandishi. Barua rasmi huweza kutumika kutoa taarifa, kuomba kazi, kuagiza bidhaa au vitu mbalimbali vilivyo mbali, au kutoa mwaliko wa sherehe au hafla tofauti tofauti. Dhima za Barua rasmi
- Huwezesha mtu kupasha habari au taarifa kwa njia iliyo rasmi na fupi, kwa mfano barua za mwaliko wa sherehe au hafla mbalimbali
- Hufikisha taarifa zinazohusu mtu fulani kwa haraka,mfano barua za maombi ya kazi.
- Huweza kutumika kama kumbukumbu za baadae kwenye kazi za kiofisi
Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa Barua Rasmi
- Anwani ya Mwandishi
Huandikwa juu upande wa kulia wa barua, kimuundo anwani ya mwandishi huwa katika umbo la mshazari. Anwani ya Mwandishi ndio atakayotumia mwandikiwa wa barua pale atakapohitajika kujibu barua.
- Tarehe
Huandikwa chini kidogo ya anwani ya mwandishi baada ya kuvuka nafasi moja ya karatasi.
- Namba ya kumbukumbu ya barua
Hutakiwa kuandikwa kwa ufupi, katika uandishi wa barua rasmi namba ya kumbukumbu ya barua hurahisisha urejeaji wa barua za zamani ambazo huhifadhiwa katika majalada.
- Anwani ya mwandikiwa wa barua
Anwani hii huandikwa upande wa kushoto wa barua chini ya namba ya kumbukumbu ya barua. Katika muundo wake hutakiwa kuwa wima na sio mshazari kama anwani ya mwandishi.
- Mwanzo wa barua
Hukaa upande wa kushoto wa barua chini kidogo ya anwani ya mwandikiwa, mwanzo wa barua rasmi hutaja wadhifa alionao anayeandikiwa barua. Kwa mfano; Ndugu Mzazi…. Au Ndugu Mkurugenzi.
- Kichwa cha barua
Huandikwa kwa herufi kubwa kwa kutumia maneno machache, hukaa katikati ya barua chini kidogo ya mwanzo wa barua, hupigiwa mstari baada ya kuandikwa.
- Utangulizi wa barua
Hukaa chini kidogo ya kichwa cha barua, haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kwa ufupi kusudi kuu la barua, huwa kama kidokezo cha barua.
- Kiini cha barua
Kiini cha barua hufuata baada ya maelezo ya utangulizi, sehemu hii ndio huelezea madhumuni ya barua au lengo lake.
- Mwisho wa barua
Sehemu hii ndio hitimisho la barua, katika sehemu hii hukaa maelezo ya msisitizo yanayolenga kutilia mkazo juu ya jambo lililoandikwa katika barua hiyo.
- Saini ya mwandishi
Saini ya mwandishi huandikwa chini kidogo ya maelezo ya barua.
- Jina kamili la mwandishi
Huandikwa chini ya saini, jina la mwandishi ndilo humuwezeshwa mwandikiwa wa barua kumfahamu mwandishi wa barua.
- Wadhifa wa mwandishi
Barua rasmi lazima ionyeshe wadhifa wa mwandishi na huandikwa baada ya kutajwa jina la mwandishi wa barua. MUUNDO WA BARUA RASMI [table][tr][td]TAREHE[/td][/tr][/table] [table][tr][td]ANWANI YA MWANDISHI[/td][/tr][/table] [table][tr][td]NAMBA YA KUMBUKUMBU YA BARUA[/td][/tr][/table] [table][tr][td]KICHWA CHA BARUA[/td][/tr][/table] [table][tr][td]UTANGULIZI[/td][/tr][/table] [table][tr][td]KIINI CHA BARUA[/td][/tr][/table] [table][tr][td]MWISHO WA BARUA[/td][/tr][/table] [table][tr][td]SAINI YA MWANDISHI MWANDISHIMWAMWANDISHI[/td][/tr][/table]
[table][tr][td]JINA LA MWANDISHI[/td][/tr][/table] MFANO WA BARUA RASMI KAMPUNI YA DAWA YA MBU, S.L.P 40052, DAR ES SALAAM, 11/11/2011. KDM/1412 MKUU WA SHULE SHULE YA MSINGI BWAWANI S.L.P 195 BUKOBA Ndugu, YAH: KUTUMIWA CHETI Tafadhali rejea barua yangu yenye kumbukumbu namba KDM/ 1412 ya tarehe 1/7/2011. Katika barua hiyo niliomba mnitumie cheti change cha kumaliza kidato cha sita, mpaka leo sijafanikiwa kukipata. Iwapo utakituma tafadhali naomba unijulishe. Natumaini ombi langu litafanikiwa. Wako Mtiifu J. G. Nyenga JOHN GEOFREY NYENGA (Mwanafunzi) Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye Kuandika Barua rasmi
- Barua iandikwe kwa maneno rasmi tu bila kuingiza utani
- Barua ieleze kusudi la ujumbe moja kwa moja
- Kuepuka kutumia lugha za kihuni au misemo ya kileo
- Ni lazima kuwe na anwani mbili, ya mwandishi na mwandikiwa.
SIMU ZA MAANDISHI Ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa haraka sana kuliko barua nyingine za kawaida. Simu hizi huandikwa kwenye fomu, fomu hizo hutolewa na shirika la posta. Simu hizi hujulikana kwa jina la telegram. Kwa kawaida simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura kwa sababu kwa kawaida simu za maandishi baada ya kuandikwa humfikia mwandikiwa kwa muda usiozidi siku tatu. Gharama za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa. MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDISHI WA SIMU YA MAANDISHI
- Anwani ya mpelekewa habari
- Taarifa au ujumbe mfupi mara nyingi huwa na maneno manne, matano mpaka kumi.
- Jina la mwandishi
- Kuandika kwa herufi kubwa
- Kutotumia alama zozote za maandishi kama mkato, nukta na nyinginezo.
- Maandishi yanapaswa kuwa ndani ya fremu.
- Maandishi hayatakiwi kuzidi maneno kumi.
Kwa mfano; Kutuma taarifa kwa Kaka yako Keneth John aliyeko Arusha S.L.P 111 aje akupokee stendi siku ya tarehe 12/12/2012 Jina lako ni Ikramu Mohamed[table][tr][td]KENETH JOHN SLP 111 ARUSHA NIPOKEE STENDI 12/12/2012 IKRAMU MOHAMED[/td][/tr][/table]
SIMU ZA MDOMO Aina hii ya simu hufikisha ujumbe kwa njia ya mazungumzo, na hazitumii muda mrefu kufikisha ujumbe. Huduma ya simu ya mkononi hutolewa mahali kokote. Kutokana naa uvumbuzi wa simu za kiganjani siku za hivi karibuni watu wengi wanamiliki simu kwahiyo kila muda anapohitaji kuwasiliana na mtu mwingine hifanya hivyo wakati wowote na mahali popote alipo. Tofauti kati ya Simu ya Maandishi na Simu ya mdomo Simu ya Maandishi
- Hufikisha ujumbe kwa njia ya maandishi
- Ujumbe huchukua mda mrefu kufika ulipokusudiwa
- Ujumbe hulenga wanaojua kusoma na kuandika tu
- Simu za maandishi hutolewa posta tu.
Simu ya Mdomo
- Hufikisha ujumbe kwa njia ya mazungumzo yam domo.
- Huchukua muda mfupi kufikisha ujumbe kwa mlengwa.
- Hulenga watu wote,wanaojua na wasiojua kusoma.
- Hutolewa popote bila kuchagua mahali.
DAYOLOJIA Ni mazungumzo au majibizano ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utungaji dayolojia inaweza kuwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au maandishi. Katika kutunga dayolojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayolojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandika dayolojia, Kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko. Wahusika wanapaswa kupangiwa majukumu kulingana na matendo yao kwa mfano kama mhusika ni mkulima ni lazima mtunzi atumie mandhari ya shambani na lazima lugha iendane na hali halisi ya mkulima. Mambo ya kuzingatia katika Kutungia Dayolojia
- Mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika mwenyewe.
- Mtunzi ajue ameandika nini na anachokiandika kinapaswa kuendana na mandhari ya mazungumzo yanapofanyika.
- Mazungumzo ya mhusikaa yanapaswa kuwa mafupi ili yasisahaulike na yasichoshe.
- Lugha ya wahusika lazima iwe na uhalisia.
- Kuwe na mwongozo kwa msomaji ili aelewe, Kwa mfano (akasimama ghafla).
- Mtunzi anapaswa kutumia vihisishi kama vile Loh!, Ati! Na vingine.
Mfano wa dayolojia (Akiwa na hasira mama anamuita binti yake) Mama: (Akiita) Rozi! Rozi ! Rozi: Nini tena? Mama: Njoo hapa haraka Rozi: (Anakuja polepole) Nimekuja aya sema Mama: Nieleze ulilala wapi jana? Rozi: Mbona wewe sijakuuliza ulilala wapi? Mama: Unasemaje??? Rozi: Kwani hujasikia? Mama: (Anahamaki) kweli mtoto wewe ni ibilisi mkubwa Rozi: Umemaliza matusi yako? Mama: Toka humu ndani nisikuone teena. BARUA NA KADI YA MUALIKO
- Barua za mialiko
Hizi ni kama zinazoandikwa ili kupeleka taarifa za kuomba mtu ahudhurie katika sherehe au harambee fulani. Barua za aina hii huwa na ujumbe mfupi sana. Mambo ya Kuzingatia Katika kuandika Barua za mialiko
- Jina la anayealika
- Jina la mwalikwa
- Kusudi la mwandishi
- Tarehe ya sherehe
- Muda utakaofanyika na mahali itakapofanyika sherehe au harambee.
- Anwani na simu ya mwandikaji kwa ajili ya kutumwa taarifa za wasiofika.
Mfano wa Barua ya Mwaliko Shule ya Sekondari Mbagala S.L.P 0507 Dar es Salaam 2/3/2011 Mratibu wa Kutokomeza Ukimwi TACAIDS, S.L.P 45 Dar es Salaam. Ndugu, YAH: MWALIKO WA KUTOA HOTUBA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MBAGALA Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu, sisi ni wanafunzi wa kidato cha katika shule ya sekondari Mbagala. Tunaomba ufike shuleni kwetu tarehe 24/4/2011 saa 4 asubuhi ili uzungumze na wanafunzi. Mada kuu ni itakuwa NAMNA YA KUISHI NA WANAFUNZI WENYE VIRUSI VYA UKIMWI DARASANI. Mkutano huo utafanyika kwenye bwalo la shule. Shule yetu ipo barabarani, Kituo cha Mbagala mwisho ukipanda gari zinazoenda kichemchem. Karibu sana Wako Mtiifu Sebastian Massawe (Simu 0719950650) Kiongozi wa darasa KADI ZA MIALIKO Ni aina ya Karatasi ngumu inayopeleka taarifa fupi kumuomba mtu ahudhurie katika sherehe fulani, kwa mfano harusi, ubatizo, mahafari na vikao mbalimbali vya sherehe. Kadi za mialiko pia huweza kuwa ya kuomba mchango kwa ajili ya sherehe fulani tofauti. MAMBO YA KUZINGATIA
- Jina la mwandishi/ mhusika wa sherehe
- Jina la mwandikiwa/mwalikwa kwa vifupisho kama vile Prof, Bw. Bi.Mr & Mrs, Dkt.
- Lengo la mwaliko
- Mahali panapofanyika shughuli
- Terehe ya shughuli
- Wakati wa shuguli
- Jina la anwani ya mtu atakayepelekewa majibu.
Mfano wa Kadi ya mwaliko[table][tr][td]MWALIKO WA HARUSI Famili ya Bwana Lukole wa Longido Arusha inayofuraha kukualika Prof/Dkt/Padre/Bwana/Bi/Miss/Mr/Mrs …………………………….. Kwenye harusi ya Mtoto wao Lomayani Lukole itakayofanyika Longido Arusha tar 29/6/2015 saa 7 mchana Kufika kwako ni muhimu Majibu kwa wasiofika John Geofrey 0717455676 0 [/td][/tr][/table]
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.